Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 11 July 2015

KIROHO SAFI KABISA !! MEMBE AMESEMA ENDAPO YEYE HATAINGIA KATIKA TATU BORA ATAKUWA TAYARI KUWAUNGA MKONO WATAKAO BAKI


Mh. Bernard Membe

Baada ya Mh. Bernard Membe kufanikiwa kuingia katika ile orodha ya tano bora kati ya wale ambao wanawania nafasi ya Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Mhemiwa Membe amesema kuwa ikiwa naye hata ingia katika kundi la watu watatu basi atawaunga mkono watakao chaguliwa.

Membe ameyasema hayo mjini Dodoma ambapo ameeleza kuwa hata kama hatapata nafasi ya kuwepo katika kundi la wale watatu watakaopatikana hapo baadaye yeye atakuwa tayari kuwaunga mkono watakao chaguliwa.

 "Hata kama mimi sitakuwepo katika kundi lile la wale watatu mtashuhudia nitakavyoanza kuwaunga mkono wale watu watakaochaguliwa kwenda kwenye mkutano mkuu na baadaye tutapata mtu mmoja"  alisema Membe.

Mhe. Membe pia amewapongeza wote walioshiriki katika mchakato huo

"Nawapongeza wote walioshirikia katika mchakato huu, kukosa katika siasa ni jambo la kawaida na ni kitu kinauma, lakini huwezi kukizuia. Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza kwa kushiriki na kuonesha demokrasia na kuwapongeza wale wote waliokubali kushindwa." alisema Mh. Membe

Pamoja na hayo Membe amewataka watanzania kukiamini chama, huku akisema kuwa " Tukiamini chama na wakati wote tujue kwamba uamuzi wa chama kuanzia mwaka 1965 hadi leo haujafanya makosa kukubali kushindwa ni sehemu ya demokrasia"
.


No comments:

Post a Comment