Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 2 July 2015

KUNA NCHI NYINGINE YA AFRIKA IMEAMUA KUHALALISHA MAPENZI YA JINSIA MOJA, JE UNGEPENDA KUIFAHAMU? IPO HAPA

Stori za kuhusu masuala la mapenzi ya jinsia moja zimekuwa zikisikika sana miaka ya hivi karibuni, lakini pamoja na kusikika huko bado nchi nyingi za kiafrika zimekuwa zikipinga sana juu ya suala hili.

Lakini katika hali ya kushangaza nchi ya Msumbiji imeamua kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja, nchini mwao na hivyo kufanya nchi hiyo kuwa moja wapo mwa nchi chache za Afrika zinazohalalisha mapenzi ya namna hiyo.

Kufuatia hatua hiyo sasa Msumbiji inajiunga na mataifa mengine ambayo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ivory Coast na Afrika Kusini, ambapo ndani ya mataifa hayo yote si hatia kujihusisha na mapenzi wa jinsia moja.

Aidha, watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja,wamesema kuwa hatua hiyo imekuwa ni ushindi mkubwa kwao.

Hata hivyo bado kumekuwepo na nchi nyingi za Afrika ambazo zimeendelea kuweka sheria kali dhidi ya mapenzi ya jinsia moja, ikiwemo Nigeria ambayo ilipiga marufuku na kuweka adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, huku Uganda nayo ikiwa imeapa kurejesha sheria kali kuharamisha mapenzi ya jinsia moja.

 Kama unahitaji kutangaza nasi kupitia tovuti hii, wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu themanini

No comments:

Post a Comment