Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 13 July 2015

KURUDISHA FURAHA YA MTOTO WAKO KWA KUMSAIDIA KUONDOKANA NA TATIZO LA KUKOSA CHOOWatoto wadogo hususani wale ambao bado wananyonya na wale ambao ndio wameanza kula vyakula vingine zaidi ya maziwa, mara nyingi hupatwa na tatizo hili la kuwa na choo kigumu na hata kukosa choo kabisa.

Kukosa choo au kupata choo kigumu ni hali ambayo kitaalam huitwa ‘constipation’ hali hii huweza kuwakuta watu wazima na hata watoto pia, lakini leo tutaangali kwa watoto.
Mara nyingi tatizo hili huwakumba watoto wale ambao tayri wanakuwa wameanza kulishwa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama.

Wataalam wanashauri tatizo hili linapomkuta mtoto wako ni vyema kwanza kumuona daktari pindi unapogundua mtoto wako anasumbuliwa na tatizo hili.

Pia unaweza kujaribu kutumia njia hizi zifuatazo ili kuondokana na tatizo hilo;

Mpatie mtoto maji safi na salama ya kutosha na utakuwa ukipunguza kiwango au kuongeza kiasi cha maji kulingana na hali ya mtoto inavyokuwa ikiendelea.

Pia unaweza kumpatia mtoto juisi za matunda pamoja na kumpa vyakula vyenye nyuzi nyuzi endapo mtoto atakuwa ameshaanza kula vyakula vigumu.

Mbali na hayo, unaweza kumpaka mwanao mafuta kidogo sehemu inayotoka choo kikubwa ili kurahisisha utokaji wa kinyesi. Hakikisha mafuta unayotumia si yale yenye madini (mineral oi

Kama una maswali au maoni unaweza kuwasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

 

No comments:

Post a Comment