Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Sunday, 26 July 2015

KWELI DAMU NZITO KULIKO MAJI OBAMA KAKUTANA NA DADA YAKE NCHINI KENYA UNAJUA KILICHOFUATA?


Ule msemo wa damu ni nzito kuliko maji ulidhirika wazi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi Kenya ijumaa usiku.

Hiyo ni baada ya rais wa Marekani Barack Obama kuweka historia kwa kuwa kiongozi wa kwanza wa taifa lenye nguvu zaidi duniani kukanyaga ardhi ya Kenya, lakini picha zilizosambaa kote duniani zilikuwa za rais Obama akimkumbatia mwanamke aliyekuwa mwisho kabisa katika foleni ya wale waliomkaribisha nchini humo wakiongozwa na mwenyeji wake rais Uhuru Kenyatta.


Mwanamke huyo aliyepigwa picha na rais Obama na hata wakaondoka naye katika gari lake maalum al maarufu ''The Beast'' alikuwa  si mwengine bali ni dada yake wa kambo wa rais Obama aitwaye Daktari Auma Obama.

Rais Obama alimbusu bi Auma Obama na kuzungumza naye kwa muda mrefu huku rais Uhuru Kenyatta akimsubiri.

Zaidi ya hayo, Auma aliruhusiwa na maafisa wa usalama kutoka Marekani kuingia ndani ya gari maalum la rais Obama  ''The Beast''. na kuwaacha Wakenya wengi na watu wengi vinywa wazi kwani awali hawakujua mwanamke huyo alikuwa ni nani.

Dkt Auma pia alipata fursa ya kuingia kwenye gari maalum la rais Obama
 Dkt Auma yeye amesomea masuala ya sanaa na anapenda kuwasaidia watu wasiojiweza katika jamii, hata hivyo Dkt Auma licha ya kuwa na uhusiano na rais mwenye ushawishi mkubwa zaidi duniani, anapenda kuendesha shughuli zake za kibinafsi zaidi.

No comments:

Post a Comment