Thursday, 30 July 2015

KWELI WATU HAWAKATI TAMAA HIVI UNAWEZA KUAMINI KUWA HADI LEO ILE NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA BADO ILIKUWA INATAFUTWA? TAARIFA MPYA ZIMEPATIKANA ZIPO HAPA


Bila shaka kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa taarifa mbalimbali kupiti redio, luninga au magazeti basi utakuwa unaikumbuka ile story ya kuhusu ile ndege ya Malaysia iliyopotea ikiwa na abiria wake wapatao 239.

Sasa Mamlaka ya usafirishaji nchini Ufaransa imesema kuna mabaki yamepatikana ndani ya bahari ya Hindi na huenda yakawa ni mabaki ya ndege ya Malaysia ya MH370 iliyopotea bila kuwa na taarifa zozote kwa muda mrefu sasa.

Taarifa kutoka Marekani zinasema wachunguzihao ambao wameona picha za mabaki hayo wana uhakika mkubwa kwamba ni ya ndege hiyo ya Malaysia ambapo mabaki hayo ni sehemu ya bawa la ndege.

Hata hivyo, Wataalamu wa Ufaransa wanasema ni mapema mno kutoa uhakika kwamba mabaki hayo ni lazima yatakuwa ya ndege ya Malaysia aina ya Boeing 777 ambayo kupotea kwake kumeleta gumzo la kidunia.

Akizungumza mjini New York Marekani, Waziri wa Usafirishaji wa Malaysia Liow Tiong Lai amesema nchi yake imetuma wataalamu zaidi kuchunguza mabaki hayo.

"Tunahitaji kuthibitisha" amekaririwa akisema Waziri Lai,na kusisitiza kuwa kwa vyovyote vile, mabaki yaliyopatikana yanahitaji kuhakikishwa kabla ya kuthibitisha zaidi kama ndio hasa mabaki ya MH370.

Unaweza kutangaza na tovuti hii sasa wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment