Tuesday, 21 July 2015

LIST YA VYAKULA MUHIMU VYA KUZINGATIA KULA WAKATI WA UJAUZITO


Lishe bora wakati wa ujauzito ni muhimu kwa ajili ya afya yako na maendeleo ya mtoto anayepo tumboni.

Zifuatazo ni dondoo muhimu za kukuwezesha uwe na lishe nzuri wakati wa ujauzito:
  1. Kwanza hakikisha unapata mlo kamili kila siku kwa kupata vyakula vya protini, wanga, vitamin, mafuta, madini na maji ya kutosha.
  2. Kula sana matunda na mboga za majani. Ikiwezekana nusu ya mlo wako iwe ni matunda na mboga za majani 
  3. Tumia nafaka zisizokobolewa kama unga wa dona au mtama, mchele usiokobolewa, mikate ya brown.
  4. Chagua vyanzo vyako vya protini zaidi katika samaki, kuku, mayai, jamii ya maharage, soya na karanga.
  5. Kunywa maji yakutosha kila siku, zisipungue lita 2.5 kwa siku.
  6. Mazoezi pia ni muhimu, unaweza kutembea kwa dakika 30 kwa siku.
  7. Acha au epuka matumizi ya pombe kwani huathiri afya ya mtoto tumboni
Kama unahitaji kuwasiliana na Dk Abdallah Mandai unaweza kumpigia simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com pamoja na ukurasa wa facebook uitwao Mandai Herbalist Clinic- mhc

No comments:

Post a Comment