Thursday, 30 July 2015

LOWASSA KUCHUKUWA FOMU YA URAIS LEO APEWA RUHUSA YA KUJA NA MBWEMBWE ZOZOTE ATAKAZOPENDA

Mwanachama mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward Lowassa anatarajia kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na cahama hicho kugombea nafasi ya urais.

Akizungumza hapo jana jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA ( Zanzibari) Salum Mwalimu, alisema Lowassa atachukua fomu hizo leo kuomba ridhaa ya chama hicho na baadaye ya UKAWA aweze kugombea urais.

"Kesho (leo) saa tano asubuhi Lowassa atachukuwa fomu ya urais na tunamweka huru kuja kwa namna yoyote ile. Akitaka kuja na mdundiko haya! Akija na matarumbeta sawa, akiamua kwenda kwetu Zanzibar na kuja na 'mauled' pia tunamruhusu, alisema Mwalimu.

Hatua hii ya kuchukua fomu ya kuwania urais itakuwa ni mara ya tatu kwa Lowassa kuchukua fomu kwa lengo la kusaka nafasi hiyo ya juu zaidi nchini. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1995 na kufuatiwa na mwezi Juni mwaka huu akiwa ndani ya chama chake cha awali cha CCM kabla jina lake halijakatwa na vikao vya juu vya chama hicho na kuamua kuhamia CHADEMA.

Unaweza kutangaza na tovuti hii sasa wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment