Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 1 July 2015

MAFURIKO YASABABISHA VIFO VYA WATU 28 NCHINI CHINA


Kama ulikuwa unadhani kuwa mafuriko huwakumba wakazi wa Jangwani (Tanzania) tu, basi jua haupo sahihi

Leo nina hii taarifa ambayo si nzuri kutoka nchini China ambapo watu 28 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na mvua kali, zilizopelekea mafuriko na mmomonyoko wa ardhi.

Kufuataia hali hiyo imeelezwa kuwa wengine hawajulikani walipo kufuatia mvua kali zinazonyesha kwa muda wa siku 4 na kupelekea mafuriko na mmomonyoko wa ardhi nchini humo.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Shangcheng kutoka mji wa Henan, lilifahamisha kuwa watu watano wanaripotiwa kufa na wengine 800 walihama miji yao huku majengo 100 yakiharibika na zaidi ya 200 kujeruhiwa.

Mvua hizo zimesababisha kutokea kwa hasara ya kiuchumi ya Yuan milion 305, na uharibifu wa hekta 6,700 za mazao na uharibifu wa miundombinu ya umeme hususani nguzo.

Shukrani kwa kuendela kuungana nasi mdau wetu, pia tunapenda kukukaribisha kutangaza biashara yako kupitia website hii, gharama zetu ni nafuu sana. Tupigie simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. 
 

No comments:

Post a Comment