Tuesday, 21 July 2015

MAGONJWA YA ZINAA NI HATARI, LEO UFAHAMU HUU UGONJWA WA PANGUSA PAMOJA NA DALILI ZAKE


Wiki hii nimekuwa nikizungumzia sana kuhusu magonjwa ya zinaa, hivyo naomba niendelee kuzungumzia magonjwa hayo na leo nitazungumzia kuhusu ugonjwa wa pangusa.

Pangusa ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria ambao huleta vidonda vyenye maumivu sehemu za siri. Husababishwa na bakteria aina ya 'Haemophilus ducreyi.'
Ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya ngono peke yake, lakini pia kupata ugonjwa huu unakuwa upo kwenye nafasi kubwa ya kupata VVU.

Mara nyingi dalili za magonjwa haya ya zinaa huwa hazitofautiani sana, hivyo ugonjwa huu wa pangusa dalili zake ni mhusika kuhisi maumivu wakati wa kukojoa, maumivu wakati wa kufanya mapenzi kwa wanawake na kupata kidonda chenye maumivu sehemu za siri.

Kidonda hicho mara nyingi huanza kama kipele ambacho hukaa kwa siku 4 hadi 7 na baadae kupasuka kuwa kidonda. Kinakuwa na maumivu, usaha au kutoa damu pale kinapotoneshwa.

Ili kuepuka ugonjwa huu ni muhimu sana kutumia kondom kila unaposhiriki ngono au itakuwa vizuri zaidi endpo utaamua kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu. Pia kama unasumbuliwa na magonjwa haya ya zinaa unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic ambapo utapata dawa asilia zitokanazo na mimea na mitishamba. Wasiliana nasi sasa kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment