Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 20 July 2015

MAJAMBAZI YALIYOUA STAKISHARI YAKAMATWA


Ilikuwa ni usiku wa July 12, 2015 ambapo majambazi walivamia Kituo cha Polisi Stakishari Ukonga, jijini Dar es Salaam, tukio ambalo lilisababisha vifo vya watu 7 wakiwemo pia askari wanne na watu wengine watatu.

Taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ni kwamba kuna watu watano wamekamatwa wakihusishwa na tukio hilo na pia kuna silaha ambazo zimekamatwa, ziko Bunduki 15 pamoja na risasi 28 ambazo zote ni sehemu ya zilizoibiwa wakati wa tukio la Ujambazi uliofanyika Stakishari pamoja na jumla ya pesa ya milioni 170.

No comments:

Post a Comment