Friday, 31 July 2015

MAMBO AMBAYO YANAONGEZA UWEZEKANO WAKUPATA SHINIKIZO KUBWA LA DAMU


Shinikizo kubwa la damu ni ongezeko la nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa inayochukua damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye viungo na tishu mwilini.


Kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu mwilini ni 120/80mmHg au chini yake. Pale kiwango kinapokuwa 140/90mmHg au zaidi hali hiyo huwa ni shinikizo kubwa la damu.

Tatizo hili kwa kawaida huwa halina dalili za wazi zinazojitokeza pale ambapo una shinikizo kubwa la damu linatokea.

Mambo yanayoongeza uwezekano wa kupata shinikizo kubwa la damu ni haya yafuatayo:

  • Kuwa na historia ya shinikizo la kubwa la damu katika familia yako
  • Kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40
  • Kuwa na jinsia ya kiume, kwasababu huwapata wanaume zaidi kuliko wanawake
  • Kuwa na uzito uliozidi kiasi
  • Kuwa na msongo wa mawazo (stress)
  • Kuwepo na matatizo mengine ya kiafya mwilini, kama magonjwa ya figo, matatizo ya mishipa ya damu, magonjwa ya moyo, kisukari au saratani
  • Matumizi ya chumvi kwa wingi au vyakula vyenye chumvi nyingi
  • Matumzi ya baadhi ya dawa
  • Utumiaji wa pombe na uvutaji sigara
  • Ujauzito
 Kwa maelezo zaidi au ushauri kuhusu magonjwa na tiba asilia kwa ujumla basi wasiliana nasi sasa kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment