Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Wednesday, 1 July 2015

MAMBO MATANO YAKUZINGATIWA WAKATI WA KIPINDI CHA UJAUZITO


Mwanamke anapokuwa mjamzito huhitaji uangalizi wa pekee na namna yake tofauti na pale anapokuwa si mjamzito.

Kwanza kabisa mama mjamzito anapaswa kula chakula chenye virutubisho vya kutosha pamoja na madini ya chuma, hii ni kwa sababu madini hayo ya chuma husaidia ongezeko la damu mwilini hivyo kumsaidia mwanamke pale atakapokuwa amepoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.

Kipindi cha ujauzito mama hupaswa kuepuka maambukizo katika mlango wa kizazi na sehemu za siri na pale inapotokea akapata maambukizi kama hayo ni vyema akapata matibabu sahihi mapema zaidi.

Mama mjamzito anapaswa kuepuka matumizi ya pombe na dawa za kulevya, matumizi ya vilevi hivyo huhatarisha afya ya mtoto na huweza kuchangia mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu, hivyo wataalam wa afya hupendekeza mama mjamzito asinywe pombe hata kwa kiwango kidogo.

Mama mjamzito hupaswa kuepuka kutumia dawa ovyo pasipo maelekezo maalum ya daktari

Mbali na hayo, pia mama mjamzito anatakiwa kuepuka kuwa na uzito kupita kiasi pamoja na kuzingatia usafi wake binafsi ambao ni wa kawaida tu kama vile kudumisha kunawa mikono na kuosha vyakula kabla ya kula

Shukrani kwa kuendela kuungana nasi mdau wetu, pia tunapenda kukukaribisha kutangaza biashara yako kupitia website hii, gharama zetu ni nafuu sana. Tupigie simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. 
No comments:

Post a Comment