Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 15 July 2015

MGOMBEA URAIS WA UKAWA KUFAHAMIKA NDANI YA SIKU SABA

Ikiwa tayari Watanzania wameshamtambua mgombea urais kwa tiketi ya CCM ambaye ni Mh. John Magufuli UKAWA nao wamesema wanatarajia kumtangaza mgombeo wao wa urais kwa shamrashamra ndani ya siku saba.

Akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia amesema kuwa taratibu zote zimekamilika ndani ya vyama vinavyounda UKAWA na kilichobaki ni jinsi gani ya kumtangaza mgombea urais ndani ya UKAWA kwa kushirikiana na vyama vyote vinavyounda umoja huo, ndani ya siku saba .

Aidha, Mbatia alitumia nafasi hiyo kuwasisitiza watanzania kuwa wavumilivu na kuwataka wajitokeze kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura linalotegemea kuanza punde katika mkoa wa Dar es Salaam, huku wakitega masikio yao na kumpokea mgombea urais ambaye atatambulishwa kuipeperusha bendera kupitia UKAWA.

Karibu utangaze nasi sasa wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu tisini.

No comments:

Post a Comment