Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 7 July 2015

MRAMBA NA YONA MIAKA MITATU JELA

Moja ya taarifa kubwa katika magazeti mengi  Tanzania leo ni ile stori ya Basil Pesambili Mramba na Daniel Yona ambao walikua mawaziri katika serikali ya awamu ya tatu, baada ya Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam kuwahukumu miaka mitatu jela.

Basil Mramba alikuwa ni Waziri wa Fedha na uchumi na Daniel Yona alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa utawala wa Rais Benjamini Mkapa.

Kutoka kushoto ni Basili Mramba, Daniel Yona na Gray Mgonja
Mawaziri hao wamehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela jana tarehe 6 mwezi Julai kwa kuisababishia serikali hasara ya bilioni 11.7 pamoja na utumiaji mbaya wa madaraka.

Aidha hukumu hiyo imeambatanishwa na faini ya shilingi milioni tano kwa kila mmoja wao.

Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja ameachiwa huru baada ya kutokua na hatia yoyote ile.

No comments:

Post a Comment