Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 8 July 2015

MWANAUME MZEE ZAIDI DUNIANI AFARIKI DUNIA


Mwanaume mzee zaidi duniani raia wa Japan aliyefahamika kwa jina la Sakari Momoi ameaga dunia mjini Tokyo akiwa na umri wa miaka 112.

Mwanaume huyo ambaye aliwahi kuwa mwalimu mkuu wa zamani wa shule ya upili na baba wa watoto watano, aliaga dunia kutoka na ugonjwa wa figo katika kituo kimoja cha kuwahudumia watu wazee siku ya Jumapili.

Momoi alizaliwa mwaka 1903 mjini Fukushima na alikuwa mwalimu kabla ya kupanda cheo na kuwa mwalimu mkuu kwenye shule kadha nyumbani kwao.

Alikuwa na mazoea ya kusoma hasa mashairi ya Kijapan na pia alipenda kusafiri sehemu mbali mbali nchini Japan na mkewe ambaye sasa pia marehemu.

Itakumbukwa kwamba mwezi Aprili mwaka huu pia mtu mzee zaidi na mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani Misao Okawa kutoka Japan aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 117 na sasa rekodi inashikiliwa na mmarekani Susannah Mushatt Jones ambaye ana umri wa miaka 116.

Mtu ambaye aliishi miaka mingi zaidi duniani kulingana na Guinness ni Jeanne Calment kutoka ufaransa ambaye aliishi miaka 122 na siku 164 na aliaga dunia mwezi Agosti mwaka 1997.

 Kama unahitaji kutangaza nasi kupitia tovuti hii, wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu tisini.

No comments:

Post a Comment