Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 7 July 2015

NDEGE YATUA KWA DHARURA KISA NI TABLET TU!!Kweli kuna baadhi ya makampuni wako makini sana na kazi zao na hakuna kitu cha kupuuza endapo mambo yanakuwa hayajafanyika katika mpangilio maalum.
 
Kuna hii taarifa ya ndege ya shirika la Turkish Airlines iliyokuwa safarini ikielekea Uingereza ikitokea jijini Istanbuln yenyewe ililazimika kutua kwa dharura baada ya kuonekana kwa "tablet" ambayo haikuwa imeorodheshwa katika idadi ya mizigo ya ndege hiyo. Jambo ambalo kwa mashirika mengine huenda wangepuuza tu nakuendelea na safari.

Lakini Rubani wa ndege hiyo baada ya kufahamishwa habari hiyo aliwasiliana na maafisa katika uwanja wa ndege wa Belgrad nakuelekezwa namna ya kutua.
Ndege ya Shirika la Turkish Airlines
Wasafiri katika ndege walifikishwa katika eneo salama walipotua katika uwanja huo na kikosi cha kulinda usalama kikafanya uchunguzi wake.

Baada ya uchunguzi huo nchini Serbia, ndege hiyo ilianza tena safari yake na kuelekea London nchini Uingereza.

Kama unahitaji kutangaza nasi kupitia tovuti hii, wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu themanini

No comments:

Post a Comment