Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 27 July 2015

NI NGUMU SANA KUZIMALIZA FAIDA ZOTE ZA TANGAWIZI KIAFYA, LEO KUNA HIZI NYINGINE NIMEKULETEA


Tangawizi ni moja ya kiungo ambacho hutoa ladha nzuri sana kwenye chai au hata chakula pia, lakini kiungo hiki kina umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu

Tunaposema tangawizi inaumuhimu mkubwa kiafya ni kutokana na uwezo wake wa kutibu matatizo kadhaa yanayomkabili mwanadamu.

Miongoni mwa matatizo au magonjwa ambayo huweza kutibiwa kwa kuzingatia matumizi ya tangawizi ni pamoja kutuliza maumivu ya tumbo yatokanayo na matatizo ya mfumo mfumo mbaya wa usagaji wa chakula hivyo kwa kutumia tangawizi husaidia kuimarisha mfumo wa usagaji chakula.

Tangawizi pia inaelezwa kuwa na uwezo mzuri wa kuwasaidia wale wenye matatizo ya kuzongwa na hali ya kichefuchefu na kutapika mara kwaa mara, hivyo inaweza kuwa nzuri kwa kinamama wajawazito.

Aidha tangawizi pia inauwezo mzuri wa kuondosha mafua, lakini pia kuzibua mfumo wa hewa pale unapokuwa umeziba huenda kwa sababu ya tatizo la mafua.

Tangawizi pia inauwezo mzuri wa kutumika kama kituliza maumivu, kwani huondoa maumivu ya misuli, kichwa, na kuwasaidia hata wale wanawake ambao hupatwa na maumivu wakati wa hedhi.

Pamoja na hayo, tangawizi pia husaidia kuongeza nguvu za kiume kwa kutibu tatizo la mwanamume kutoa shahawa haraka.

Kwa maelezo zaidi au ushauri unaweza  kuwasiliana na Tabibu Abdallah Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment