Thursday, 16 July 2015

NCHINI URUSI WAO WAMEANDAA HILI SHINDANO MAALUM LA KUNG'ATWA NA MBU

Kwa hali ya kawaida watu wengi huwa tunawachukia sana mbu kutokana na ule uwezo wao wa kutusababishia ugonjwa wa malaria, lakini huko nchini Urusi mbu husheherekewa kwa tamasha la kipekee katika mji mmoja.

Katika hafla kusheherekea siku hii huandaliwa mashindano ya kuchagua msichana mrembo zaidi, ambapo wasichana hao huhukumiwa kulingana na idadi ya alama za kuumwa na mbu baada ya kusimama kwa muda wa dakika 20 wakiwa wamevalia suruali fupi na fulana ndogo.

Mshiriki wa mashindano hayo akiwa katika muonekano wa mbu
Baada ya shindano hilo jopo la majaji wataalamu wakiwemo madaktari huikagua miili ya washiriki na ushindi huenda yule atakaye kuwa na alama nyingi za kuumwa na mbu, alisema mratibu wa sherehe hiyo Natalya Paramonova.

Mbali na kushindana kuumwa na mbu hao, pia shindano hilo hushindanisha watu kushika mbu aliye hai.

Karibu utangaze nasi sasa wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu tisini.

No comments:

Post a Comment