Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 1 July 2015

NYOKA MWENYE HIRIZI ALETA TAHARUKI MKOANI MOROGORO AKUTWA MLANGONI AKIWA AMETAPAKAA DAMU MAMIA WAJITOKEZA KUMSHANGAA


Nyoka wa ajabu akiwa kwenye kizingiti cha mlango, huku akichuruzika damu
Na: Ahmad Zilkhery,  Morogoro
Hili ni tukio la kushangaza na la aina yake hasa katika huu mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, ambapo amekutwa nyoka amekufa, huku akichuruzika damu nyingi kwenye kizingiti cha mlango wa sebuleni kwa mama mmoja aliyefahamika kwa jina la mama Asma.

Tukio hilo limetokea jana katika Manispaa ya Morogoro mjini katika mtaa wa K/ ndege kata ya K/ ndege ambapo katika hali isiyo ya kawaida nyoka huyo alikutwa akiwa ameshakufa, huku akiwa na hirizi kubwa nyeusi eneo la karibu na kichwa chake na damu nyingi sana ikiwa imetapakaa eneo lote la mlangoni na Sebuleni ambapo haikua rahisi kuitambua kua ni damu ya nini. Jambo lililosababisha mamia ya wakazi wa mji huo kufurika eneo la tukio.
Mama Asma anayeishi kwenye nyumba hiyo yenye  mauzauza
Akizungumzia tukio hilo mtoto wa kiume wa mama Asma mwenye umri wa miaka 12 aliye fahamika kwa jina la Amani amesema usiku walipo amka kula daku hawakumuona nyoka huyo, lakini waliona damu imetapakaa sebuleni kote hali iliyo sababisha kuingiwa na hofu, ambapo baba wa familia hiyo aliamuru kuchukua dawa ya kienyeji na kujipaka kabla ya kwenda kulala.

Hapa tazama kipande cha video hii mtoto huyu akaielezea namna ilivyokuwa...

Katika hatua nyingine majirani walimtaka mama Asma kuhama nyumba hiyo kufuatia mauzauza anayoyapata katika nyumba hiyo, lakini pamoja na ushauri huo mama Asma alikataa kuhama na badala yake alimwita mtaalamu ili aague nyumba hiyo mali ya bwana mmoja anaetajwa kuwa ni Mmasai.

Mama Asma anasema kuwa hawezi kuhama katika nyumba hiyo pamoja na mauzauza hayo kwa kile anachodai kuwa na uhuru mkubwa wa kuishi hapo bila bughudha kwa sababu mwenye nyumba hiyo haishi hapo wala huwa hafiki hapo mara kwa mara.
Wakazi wa eneo hilo wakiwa nje ya nyumba anayishi mama Asma kwa lengo la kushuhudia nyoka huyo

Mbali na hayo mama huyo alisema nyumba hiyo imekuwa imekuwa na matukio ya ajabu mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuonekana kwa chura mkubwa mwenye nywele mithili za binaadamu kichwani, huku akidai kuwa chura huyo amekua akionekana nyakati za usiku akiranda randa ndani ya nyumba hiyo.

Itakumbukwa kwamba katika kata ya K/ndege mwaka mmoja umepita tangu lilipotokea tukio kama hilo la maajabu ambapo nalo lilihusishwa na imani za kishirikina, ambapo alitolewa mtoto mwenye umri wa miaka 4 toka ndani ya boksi la mbao alilohifadhiwa kwa miaka 4.


Endelea kuwa karibu nasi kila siku kwa habari mbalimbali kutoka hapa nchini, pia unaweza kuwasiliana nasi kama unahitaji kutangaza nasi, tupigie simu namba, 0716 300 200 / 0784 300 300 Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment