Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 4 July 2015

ORODHA YA WABUNGE WENGINE 35 WALIOSIMAMISHWA KUINGIA BUNGENI KWA SIKU TANO LEO JULAI 4, 2015


Wiki hii inayoisha Bunge halikuwa linakwenda vizuri kutokana na kuibuka vurugu katika vikao vyake vurugu ambazo zilichangia baadhi ya wabunge kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge.

Hali hiyo ya kutoelewana imeshatokea zaidi ya mara tatu ndani ya vikao hivyo vya bunge na kusababisha mara nyingine kuhairisha vikao hata kabla ya wakati.

Leo tena Julai 04, 2015 hali imeendelea kuwa hivyo hivyo mara baada ya Mbunge Ezekiel Wenje kuomba ufafanuzi wa kwanini Mbunge Silinde hayupo kwenye orodha ya waliotajwa kusimamishwa, lakini askari wa bunge wamemzuia asiingie kwenye kikao?

Majibu ya Spika hayakuwaridhisha baadhi ya wabunge na kusababisha kuanza kwa kelele na hapo ndipo spika akataja orodha ya wabunge wengine ambao wanasimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa siku tano kila mmoja.

Miongoni mwa wabunge hao waliotajwa ni pamoja na Ezekiel Wenje, Mussa Kombo, Masoud Abdallah Salim, Rebecca Ngodo, Sabrina Sungura, Khatib Said Haji, Maulidah Anna Valerian Komu, Cecilia Pareso, Kulikoyela Kahigi, Israel Natse, Khatibu Said Haji, Kombo Khamis Kombo, Ali Khamis Seif, Haroub Mohammed Shamisi

Wengine ni Kuruthum Jumanne, Joyce Mukya, Suleiman Bungura, Rashid Ali Abdallah, Ali Hamad, Riziki Juma, Dr. Anthony Mbassa, Mariam Msabaha, Grace Kiwelu, Mustapha Akonaay, Konchesta Rwamlaza, Rukia Kassim Ahmed, Azza Hamad, Mchuchuli, Amina Mwidau, Mkiwa Kimwanga, Salum Baruhani, Marry Stellah Malaki, Rashid Ally Omary, Mwanamrisho Abama na Lucy Owenya.

Kama unahitaji kutangaza nasi kupitia tovuti hii, wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu themanini

No comments:

Post a Comment