Thursday, 16 July 2015

SABABU ZINAZOCHANGIA MWANAMKE KUSHINDWA KUSHIKA MIMBA

Zipo sababu nyingi sana zinazofanya mwanamke asiweze kushika mimba kama vile kupata maambukizi katika viungo vya uzazi, hali duni ya lishe na kukumbwa na magonjwa sugu.

Wanawake wengine wanakuwa na matatizo yanayohusu upevushaji wa mayai ambayo kitaalamu huitwa ‘Ovulatory’. Tatizo hili huathiri wanawake kwa kiasi kikubwa ambapo mwanamke anapata siku zake kama kawaida lakini hapevushi mayai.

Hali hiyo husababishwa na matatizo katika mfumo wa homoni mwilini, tatizo linaweza kutokea lenyewe kutokana na mabadiliko ya mwilini.

Lakini pia tatizo hilo linaweza kujitokeza kutokana na matumizi yanayohusiana na dawa za homoni kutumika kiholela bila kupata ushauri wa daktari na ndiyo maana tunasisitiza kuwa si vema kunywa dawa bila kushauriwa na daktari.

Wanawake wengine wanaweza kushindwa kupata mimba kutokana na matumizi ya baadhi ya vyakula au vipodozi vyenye kemikali.

Matatizo mengine yanayosababisha mwanake asipate mimba ni kuwa na matatizo kwenye mirija kwani inaweza kuziba, kutanuka au kuweka usaha au maji. Maambukizi katika mirija au upasuaji wa mimba nje ya kizazi au kufunga kizazi kunaweza kumfanya mwanamke asipate mimba.

Kama wewe ni mmoja kati ya wale wanaosumbuliwa na tatizo la kupata ujauzito ni vizuri ukafika Mandai Herbalist Clinic kwaajili ya kupata matibabu pamoja na dawa ambazo zitakusaidia kushika mimba haraka pindi tu utakapoanza kutumia. Wasilina nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe (email) dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment