Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 6 July 2015

SAFARI NYINGNIE YA KUELEKEA URAIS YAANZA VIZURI KWA DK SHEIN


Dk Ali Mohamed Shein

Dk Ali Mohamed Shein amefanikiwa kuteuliwa kuwania tena kiti cha Rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu.

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Vuai Ali Vuai, alisema wajumbe kwa kauli moja wamependekeza jina la Shein kuwania nafasi hiyo baada ya kuridhishwa na utendaji wake unaotokana na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010/2015 kwa vitendo katika maeneo yote muhimu.

Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilali (kushoto) akimpongeza Dk Ali Mohamed Shein baada ya kupitishwa na Kamati Maalum ya CCM Zanzibar kugombea tena urais kwa kipindi cha pili (Picha na Ikulu)
Alisema utekelezaji huo umeiwezesha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupata mafanikio katika maeneo mbalimbali ya bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2015-2016 ikiwemo kuweka kipaumbele kwa miradi ya jamii pamoja na maendeleo.

Kwa upande wake Dk Shein ameshukuru na kukipongeza kikao hicho cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM -Zanzibar kwa kufanikisha kazi hiyo muhimu na nzito kwa mafanikio makubwa na kuahidi kuwa ataendelea kuwa mwadilifu na mwaminifu mbele ya CCM, jamii nzima ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla.

Kama unahitaji kutangaza nasi kupitia tovuti hii, wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu themanini

No comments:

Post a Comment