Tuesday, 28 July 2015

SAFARI YA LOWASSA SASA IMEKUWA RASMI ATANGAZA KUHAMIA CHADEMA WAZI WAZI ASEMA CCM ILIBAKA DEMOKRASIA DODOMA


Baada ya uvumi na tetesi za mara kwa mara kuhusu aliyekuwa Waziri Mkuu Edward  Lowassa kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA hatimaye hivi punde Lowassa ametangaza rasmi kujiunga na chama hicho.

Akitangaza uamuzi huo Lowassa amesema kuwa uchaguzi wa kumteua mgombea wa kupeperusha bendera ya CCM ngazi ya urais uliofanyika mjini Dodoma ulifanyika kwa upendeleo na chuki dhidi yake na kufafananisha kuwa hali hiyo ilikuwa ni 'sawa na kubaka demokrasia' alisema LowassaKatika hatua nyingine Lowassa amesema "kuwa yaliyotokea Dodoma yameitia dosari nchni yetu ni dhahiri kuwa CCM imepotoka na kupoteza muelekeo wa kuendelea kuiongoza nchi yetu na mimi kama mtanzania mwenye uchungu wa nchi yangu nasema kwamba CCM sasa basi"

Kufuatia maamuzi hayo Lowassa mmesema baada ya kutafakari kwa kina na kujiridhisha ameamua kujiondoa CCM na kuitikia wito wa UKAWA kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA.

Pamoja na hayo, Lowassa amesema alinyimwa haki yake na CCM kama Mtanzania kujieleza na kujitetea, hivyo atakua mnafiki akisema ana imani na chama hicho.

No comments:

Post a Comment