Thursday, 2 July 2015

SIASA BWANA!! LEO HII HATA ZILE BARABARA ZETU ZA MITAANI NAZO ZIMEONEKANA!! KWELI WATU WANAMALIZIA KUTIMIZA AHADI ZAO..

Huu muda tuliopo kwa sasa tunaweza kusema kama ni muda wa lala salama kwa wanasiasa wengi hapa nchini hususani katika kutimiza zile ahadi walizoahidi kuzitimiza ndani ya miaka mitano iliyopita ambayo ndiyo inaelekea ukingoni hapo ifikapo mwezi Oktoba.

Nimeona leo nikupe hizi picha 4 ambazo zinaonesha namna barabara zilivyoaza kukumbukwa kwa kufanyiwa marekebisho kiasi.

Hii ni barabara ya ndani kabisa au unaweza sema barabara ya mtaa iliyopo maeneo ya wilaya ya Ilala katika mtaa wa Mongolandege jijini Dar es Salaam,  lakini kwa kuwa imebaki miezi miwili kabla ya kuingia katika mchakato wa uchaguzi. Basi barabara hii nayo safari hii ikakumbukwa kwa kumwagwa angalau kifusi tu kama tunavyoona hapo chini ingawaje bado hakijasambazwa na hatujui ni lini kitasambaswa maana imekuwa shida zaidi hata namna ya kupishana kwa magari.


Ningetamani na wewe mdau wangu popote pale ulipo unitumie picha ya kile kinachofanyika kwa sasa mtaani kwako au katika mkoa wako ikiwa tunaelekea katika uchaguzi. Je, kiongozi wako anamalizia ahadi zipi kwa sasa au ameshakamirisha zote? nitumie kupitia dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment