Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 10 July 2015

TATIZO LA UTAPIAMLO KWA WATOTO LAELEZWA BADO NI CHANGOMOTO NCHINI


Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Stephen Kebwe
Imeelezwa kuwa Tanzania ni kati ya nchi tatu barani Afrika zenye watoto wengi wenye utapiamlo.

Takwimu hizo zilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Stephen Kebwe alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Rukia Kassim Ahmed.

Swali la mbunge huyo, alitaka kujua serikali inachukua hatua gani mahususi za kuhakikisha inapambana na tatizo hilo la watoto kudumaa kiakili.

Akijibu swali hilo, Dk. Kebwe alisema tatizo la watoto kudumaa kiakili lipo katika nchi nyingi duniani na linatokana na ulaji duni wa vyakula vyenye virutubisho vya kutosha.

Akifafanua zaidi alisema watoto milioni 199 sawa na asilimia 33 duniani wa chini ya miaka mitano walikuwa wamedumaa hadi kufikia mwaka 2000. Huku akieleza kwamba juhudi zaidi zinafanyika ili kupunguza tatizo hilo hadi kufikia watoto milioni 161 sawa na asilimia 25 kwa mwaka 2013.

Aidha, Dk. Kebwe alisema kutokana na utafiti wa Kidemografia wa Afya wa mwaka 2010, asilimia 42 ya watoto chini ya miaka mitano walionekana kuwa na udumavu kutokana na urefu wa kimo kutolinga na umri wao.

Mbali na Tanzania, alitaja nchi nyingine zenye tatizo hilo kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Ethiopia.

Pamoja na hayo, Dk. Kebwe alitaja njia pekee ya kuondokana na utapiamlo kuwa ni wazazi kupata elimu ya kuwapatia lishe watoto wao na kuainisha kuwa ni muhimu mama kumnyonyesha mtoto wake kwa muda wa miezi sita bila kumpatia chakula kingine.

Alisema kwa sasa serikali inaendelea na utoaji wa elimu kwa jamii ili kuhakikisha watoto wanapatiwa lishe bora katika makuzi yao yote.

“Iwapo jamii itapata elimu inayotolewa na serikali kwa ajili ya kuwapatia lishe bora watoto waliopo chini ya miaka mitano ni wazi tatizo hilo linaweza kupungua kwa kiasi kikubwa” alisema Dk. Kebwe.

Karibu utangaze nasi sasa wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu tisini.


No comments:

Post a Comment