Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 2 July 2015

TUMEJALIWA MBOGAMBOGA NYINGI ZENYE FAIDA KIAFYA, LAKINI VIPI KUHUSU HII IITWAYO BROCCOL JE, UNAFAHAMU FAIDA ZAKE


Mwenyezi Mungu ametujalia mboga za majani za aina nyingi sana, mfano mchicha, spinachi, matembele n.k, lakini kuna mboga nyingine huwa tunakutana nazo masokoni na huenda tukawa tunazipita tu bila kuzinunua huenda kwasababu hatuzijui vizuri.

Kuna hii mboga iitwayo 'Broccoli' ambayo imenipa tabu kidogo kuipatia jina lake nzuri la Kiswahili chetu, lakini mboga hii hupatikana hapa nchini na ni moja ya mboga ambayo hupendelewa sana na wenzetu wahindi na hupatikana sana katika masoko yanayotembelewa sana na watu wa aina hiyo mfano kwa hapa Dar es Salaam utakutana na mboga hii maeneo ya Posta hivi.

Lakini huenda wenzetu hao wahindi wakawa wanaipenda mboga hii ya Broccoli kutokana na kuwa na sifa hizi zifuatazo:

Mboga hii kwanza inasifa ya kuwa na kiasi kikubwa cha vitamin C zaidi ya kiwango ambacho hupatikana ndani ya chungwa.
Hii ndiyo BroccolBroccol inaelezwa kuwa na uwezo wa kumkinga mtumiaji dhidi ya magonjwa ya saratani.

Mbali na hayo mboga hii ya broccoli pia inaelezwa kuwa na uwezo wa kusaidia matatizo ya vidonda vya tumbo, hii ni kutokana na kuwa na kemikali ijulikanayo Sulforaphane

Pia matumizi ya juisi ya mbogamboga hii ya broccoli husaidi sana kuimarisha na kuongeza kinga za mwili pamoja na kumsaidia mhusika kuondokana na matatizo ya kuhisi uchovu au hata kupungukiwa na nguvu mwilini. Hivyo ni vyema ukatumia juisi ya mboga hii pia.
  
Ikiwa unapenda kufahamu zaidi kuhusu somo hili au kama unasumbuliwa na magonjwa mbambali unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba, 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment