Tuesday, 21 July 2015

UKIONA DALILI HIZI BASI JUA UPO KATIKA HATARI YA KUPATA SARATANI YA TEZI DUME


Saratani ya tezi dume ni saratani ambayo hutokea katika seli za tezi dume (prostate gland) na huweza kusambaa sehemu nyingine za mwili.

Saratani hii huweza kutokea na kukaa muda mrefu bila kuonesha dalili zozote mpaka pale inapokuwa umekua sana.

Mara nyingi dalili hutokea pamoja na matatizo mengine ikiwa ni pamoja na uvimbe wa tezi dume.

Dalili za mwanzo za mwanzo ni pamoja na mhusika kukojoa mara kwa mara hasa wakati wa usiku, mkojo kutoka kidogo au kushindwa kutoka kabisa, kupata maumivu wakati wa kutoa manii, kukojoa mkojo wenye damu pamoja na kushindwa kuzuia mkojo, hasa unapocheka.

Pamoja na dalili hizo hapo juu mtu anaweza pia kuhisi maumivu makali ya kiuno, mbavu, na kwenye mapaja, kukosa hamu ya kula, kupungua uzito, hali ya kuchoka na wakati mwingine kutapika, miguu kuvimba na wakati mwingine miguu huweza kukosa nguvu.

Unaweza kuwasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkamandaitz@gmail.com ili kupata huduma zetu, kumbuka kuwa tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment