Thursday, 30 July 2015

UKIONA DALILI HIZI HUENDA UTAKUWA NA TATIZO LA UVIMBE KWENYE KIZAZI (FIBROID)

Tatizo la uvimbe kwenye mfuko wa kizazi wa mwanamke hujulikana kama 'fibroid.' Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi.

Tatizo hili linawakuta wanawake wengi hasa walio katika umri wa miaka ya uzazi, kimsingi tatizo hili limekuwa likishuhudiwa na watu wengi pengine kutokana na watu wanavyoishi.

Tatizo hili pia huwa na dalili zake na miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na kuhisi maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi, kupata maumivu makali ya tumbo na kuhisi maumivu waati wa tendo la ndoa.

Dalili nyinyingine ni kutokwa damu isiyo ya kawaida wakati wa hedhi na zisizokuwa na mpango, kuhisi maumivu ya mgongo na kupata haja ndogo mara kwa mara kutokana na uvimbe kukandamiza kibofu cha mkojo.

Mbali na dalili hizo pia dalili nyingine ni pamoja na kutotunga mimba au mimba kuharibika na kutoka, na wakati mwingine ugumba.

Tatizo hili la uvimbe kwenye mfuko wa uzazi 'fibroids' huweza kusababisha mwanamke kushindwa kupata mtoto kwasababu uvimbe huu unapokuwa sana hukandamiza mirija ya kupitisha mayai kutoka kwenye ovari au sehemu mayai yanapotengenezwa. Uvimbe huu pia unaweza kuzuia yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi. Pia hufanya mfuko wa kizazi ukaze na hivyo kushindwa kusukuma mbegu kwenda kwenye mishipa ya kupitisha mayai.

Tunapaswa kujua kuwa wanawake wengi wana 'fibroids' ndogo ndogo lakini kwa sababu hazina dalili ni ngumu kufahamu. Kwa mantiki hiyo tunashauriwa kuwa na mazoea ya kufanya uchunguzi wa afya zetu mara kwa mara ili kuweza kushughulikia haraka matatizo kama haya.

Iwapo umeenda hospitali na ukaambiwa unasumbuliwa na tatizo hili la uvimbe kwenye kizazi na kukufanya ukashindwa kushika ujauzito basi hii ni nafasi yako ya kuwasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 8000 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili tuweze kukusaidia kumaliza tatizo hilo kwa kutumia dawa zetu za asili zitokanazo na mimea, matunda na mitishamba. Tupo Ukionga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment