Friday, 17 July 2015

VAZI LA KUFUNIKA USO LAPIGWA MARUFUKU CAMEROON

Maafisa wa serikali kaskazini mwa Cameroon wamepiga marufuku wanawake kuvaa vazi la hijabu ambalo hufunika nyuso zao.

Uamuzi huo umechukuliwa kufuatia mashambulio ya mabomu yaliyotekelezwa na wanawake waliokuwa wamevalia vazi hilo la hijabu ambao waliaminika kuwa  ni wafuasi wa kundi la Boko Haram.

Pamoja na uamuzi huo, pia Gavana wa jimbo la Far, amesema kuwa raia katika eneo hilo hawataruhusiwa kuendesha magari yenye vioo vya giza ambavyo huzuia watu kuona ndani kirahisi, huku uendeshaji wa piki piki nyakati za usiku ukipigwa marufuku.

Itakumbukwa kwamba mwezi uliopita Chad pia ilipiga marufuku wanawake kuvalia Burka.

No comments:

Post a Comment