Thursday, 30 July 2015

VIRUTUBISHO HIVI MUHIMU NDIVYO AMBAVYO UTAVIKOSA KAMA UTAACHA KULA TANGO

Siku zote huwa tunasema kwamba matunda ni kinga kwa afya yako na matunda mengi yana manufaa, lakini tango tunaweza kusema huenda linamanufaa zaidi japo wengi husema ni tunda ambalo halina ladha nzuri sana.

Tunda hili linasifika kwa kuwa na vitamin zote unazohitaji kwa siku. Kwani ndani ya tango moja kuna  vitamin B1, B2, B3, B4 na B6, madini ya chuma, 'potasium' na 'zinc'.

Aidha, tango ni msaad mzuri kwa afya ya ngozi zetu kwani husaidia sana kutoa seli zilizokufa na makunyanzi. Kinachofanyika ili kufanikisha zoezi hilo ni kusugulia vipande vya tango usoni au sehemu iliyoathirika na utaona mabadiliko mara baada ya siku chache.

Kwa wale wenye shida ya kukauka midomo nao wanaweza kutumia tango kwa kusugulia mdomo kwa utaratibu na wataona mabadiliko kwa tatizo hilo.

Kwa maelezo zaidi au ushauri kuhusu magonjwa na tiba asilia kwa ujumla basi wasiliana nasi sasa kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment