Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 28 July 2015

WALE WANAOFANYA KAZI HADI USIKU WAPO KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA WA MOYO NA KISUKARI


Taarifa ikufikie kwamba kumekuwa na utafiti ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka kadhaa miongoni mwa watu wanaofanya kazi usiku na jinsi inavyoathiri afya kwa ujumla wake.

Mwandishi Sarah Montague yeye anasema “kwa miaka kadhaa sasa nimekuwa nikiamka usiku ili kwenda kazini, hiyo ndiyo gharama ya kufanya kipindi hiki na ni kipindi ambacho nakifurahia kufanya, lakini nimekuwa nikijiuliza kama ntaathirika pakubwa kwa siku za baadae.

Mwandishi huyo anaendelea kusema kuwa “Mimi ni mmoja tu wa watu milioni 3.5 nchini Uingereza ambao hufanya kazi kwa zamu wengine wakifanya kazi kwa masaa mengi zaidi na kufanya kazi usiku wote”
Inaeelezwa kuwa watu wa zamani walikuwa wanalala kwa saa 8, lakini sasa wengi hulala saa 6 na nusu.
Watu wakitengeneza barabara usiku
Utafiti huo unaainisha kwamba hata iwapo wanaofanya kazi usiku hulala mchana, wao hulala masaa yasiyofaa.

Hata hivyo, imekuwa ikiaminika kuwa mili yetu huenda ikazoeshwa kufanya kazi usiku, lakini kwa mujibu wa mtaalamu Proff Russel Foster kutoka chuo kikuu cha Oxford, utafiti unaonyesha kuwa mwili huwa hauzoei mabadiliko hayo.

Halikadharika inaelezwa kuwa wanaofanya kazi usiku huenda wakapata magonjwa kama vile ugonjwa wa kisukari aina ya 2, ugonjwa wa moyo na hata saratani.

Pia wanasayansi wanasema mtu yeyote anayefika kazini saa kumi asubuhi huwa na uwezo mdogo wa kutatua maswala mbalimbali na huweza kufananishwa na mtu aliyekunywa pombe.

No comments:

Post a Comment