Thursday, 30 July 2015

YAFAHAMU MATUNDA HAYA YENYE UWEZO WA KUBORESHA NGOZI YAKO


Binadamu yeyote mwenye akili timamu mara zote hupenda kuonekana nadhifu na mtanashati, miongoni mwa mambo ambayo huweza kumuweka mtu kuonekana vizuri ni pamoja na suala la kuwa na ngozi nzuri.

Leo nimeona ni vyema nikakupatia huu uwezo wa matunda haya mawili yenye uwezo wa kukufanya ukaonekana vizuri hasa kwenye ishu ya ngozi. Matunda hayo si mengine bali ni papai na machungwa.

Papai

Hili ni tunda ambalo linauwezo wa kurejesha au kuziba sehemu za ngozi zilizoumia, papai pia hung'arisha ngozi na endapo kama unataka kutumia papai katika kufanya ngozi kuwa vizuri unashauriwa kuchukua papai lenyewe lililoiva kisha changanya na asali paka usoni kisha kaa nalo kwa muda wa dakika 10 baadaye safisha, fanya hivyo kwa muda wa wiki moja hadi mbili na utaona mabadiliko katika ngozi yako.

Chungwa.

Tunda hili husaidia sana kuipa ngozi uhalisa wake na namna ya kutumia ni kukamua juisi ya machungwa halafu utaitumia juisi hiyo kupaka usoni na kuiacha kwa dakika kama kumi hivi kisha osha kwa maji safi na salama, baada ya wiki kadhaa utaona mabadiliko katika ngozi yako.

Unaweza kutangaza na tovuti hii sasa wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment