Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 14 July 2015

ZIFAHAMU SABABU, DALILI NA NAMNA YA KUEPUKA SHINIKIZO KUBWA LA DAMUTunapozungumzia tatizo la shinikizo kubwa la damu, hii ni ile hali ya ongezeko la nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa inayochukua damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye viungo na tishu mwilini.

Kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu mwilini ni 120/80mmHg au chini yake. Pale kiwango kinapokuwa 140/90mmHg au zaidi hali hiyo huwa ni shinikizo kubwa la damu.

Kwa kawaida tatizo hili huwa halina dalili za wazi zinazojitokeza, licha ya baadhi yao kujisikia kuumwa kichwa mara kwa mara, kuhisi kizunguzungu, moyo kwenda kasi, kuhisi uchovu mara kwa mara au kutokwa na damu puani.

Kwa bahati mbaya sana  dalili hizo huwa ni nadra sana kuonekana kwa watu wengi hivyo watu wengi huishi na tatizo hilo kwa muda mrefu bila kufahamu.

Sababu ambazo huweza kumuingiza mtu katika tatizo hili ni pamoja na kuwa na historia ya shinikizo kubwa la damu katika familia, kuwa na umri zaidi ya miaka arobaini, kuwa  na uzito mkubwa, msongo wa mawazo (stress), matumizi ya chumvi nyingi, matumizi ya pombe na uvutaji wa sigara.

Ili kuepukana na tatizo hili ni vyema kujitahidi kuepuka kula vyakula vyenye mafuta mengi na chumvi, epuka kuwa na uzito mkubwa, epuka kula mara kwa mara nyama hasa nyama nyekundu, thibiti msongo wa mawazo pamoja na kujitahidi kushirika katika mazoezi angalau dakika 30 kwa siku.

Kama una maswali au maoni unaweza kuwasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment