Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 4 July 2015

ZIFAHAMU SABABU ZA MAUMIVU YA KIUNO NA NAMNA YA KUKABILIANA NALO


Maumivu ya kiuno ni tatizo linalowasumbua wanawake wengi mara kwa mara na mara nyingi tatizo hili hujitokeza hasa wakati wa hedhi.

Lakini kuna maumivu ya kiuno ambayo huchukuwa muda mrefu bila kutulia au kuwa yanajirudia mara kwa mara kwa muda mrefu.

Kimsingi maumivu haya huweza kuchangiwa na matatizo kwenye kibofu cha mkojo, via vya uzazi au misuli ya nyonga. Kunawakati maumivu hayo huweza kuwa makali kiasi cha kuathiri shughuli zako za kila siku.

Miongoni mwa sababu za maumivu haya ni pamoja na maambukizi ya muda mrefu ya shingo ya kizazi au mji wa uzazi ambayo husababisha maumivu ya kiuno wakati wote au wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Sababu nyingine ni kuwa na uvimbe vya kizazi ambavyo husababisha maumivu, lakini maumivu yake huwa ya kuja na kuacha. Pia tatizo hili huweza kuchangiwa na mimba kutunga nje ya  kizazi.

Pia maambukizi ya njia ya mkojo ya muda mrefu (Urinary Tract Infection). Huweza kuwa sababu ya maumivu hayo ya kiuno.

Maumivu ya kiuno pia huweza kuwasababishwa na ajali iliyoleta madhara sehemu za kiuno kwa muhusika.

Ili kupata matibabu ya tatizo hili la maumivu ya kiuno ni vizuri kwanza kugundua chanzo cha maumivu hayo kwa kufanya utafiti wa kitabibu kisha kufuatiwa na tiba.

Hivyo matibabu yatategemea sana chanzo cha tatizo, lakini kama umekuwa ukisumbuliwa na maumivu hayo kwa muda mrefu unaweza fika Mandai Herbalist Clinic ili kupata vipimo na kupata dawa nzuri zitokanazo na mimea, matunda, nafaka na mitishamba. Unaweza kuwasiliana nasi sasa kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment