Tuesday, 18 August 2015

BIDHAA HIZI HUPENDWA SANA NA WATOTO, LAKINI KUMBE NDANI YAKE HUCHANGANYWA NA BANGI

Hivi utajisikiaje endapo ukagundua kuwa zile zawadi za keki, biskuti na peremende ambazo huwa unampelekea mtoto wako kila siku zimewekwa bangi?

Sasa wizara ya afya nchini Kenya imetoa orodha ya peremende, keki na biskuti bidhaa ambazo inadai zimewekwa bangi.

Katika kile ambacho kinatarajiwa kuwashanga wazazi, barua ambayo ilitiwa sahihi kwa niaba maabara ya serikali, ilisema kuwa baadhi ya sampuli 176 zilizochukuliwa kwa peremende maarufu , keki na maandazi zilipatikana zikiwa na bangi baada ya kufanyiwa uchunguzi.

Licha ya watoto kuzipenda bidhaa hizo serikali imetaka vipigwe marufuku na kuondolewa kabisa madukani na pia wachuuzi kuzuiwa kuziuza.

Kupitia barua hiyo kwenda kwa wakuu wa afya wa kaunti zote 47 nchini Kenya, wizara ya afya imewaamrisha maafisa kukagua maduka yote, maduka ya jumla na sehemu zingine bidha hizo zinaweza kupatikana.

No comments:

Post a Comment