Wednesday, 19 August 2015

CCM WATEUA WAJUMBE 32 KUMKABILI LOWASA, IPATE LIST KAMILI HAPA

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza Kamati ya Kampeni yenye wajumbe 32, huku wengi wao wakiwa ni wale waliowahi kuvaana na mgombea wa Chadema, Edward Lowassa katika masuala tofauti.

Katika taarifa hiyo jana, CCM haikuwa na maelezo mengi kuhusu kamati hiyo zaidi ya kutangaza kuwa itaongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana na kutaja majina ya wajumbe.
“Hii ni kamati ambayo itakuwa inafanya oparations za kila siku,” alisema Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye wakati akitangaza kamati hiyo jana.
Licha ya Nape kutozungumzia majukumu ya kamati hiyo, mmoja wa wajumbe, January Makamba alisema wamejipanga vizuri na mwaka huu watafanya kampeni za kisasa.
“Tumejipanga na namna tunavyojipanga ni siri yetu, ni mambo ya ndani ambayo sisi wenyewe kwenye timu tunayafahamu na hatuwezi kutoa siri hizo kwa kuwa  ndizo silaha za maangamizi.

 Kwa kifupi tutashinda,” alisema naibu waziri huyo wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia.

Hapa kuna list ya majina ya wote waliochaguliwa katika kamati hiyo>>>


Tufikishie tangazo lako leo tuanze kukutangazie kwa gharama nafuu sana wasiliana nasi kwa simu namba 0653 163 838, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment