Tuesday, 4 August 2015

CHADEMA YAMTANGAZA RASMI LOWASSA KUWA MGOMBEA WAO WA URAIS

Mh: Edward Lowassa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo  CHADEMA kimetangaza rasmi kuwa aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa atakuwa mgombea wake wa urais wakati wa uchaguzi wa mwezi Octoba.

Uamuzi huo unafuatiwa baada ya wiki moja tangu Lowassa alipoamua kujiunga na Chadema akitokea chama tawala cha CCM.

Lowassa amekuwa CCM  kama mwanachama kwa zaidi ya miaka 30 na uamuzi wake wa kukihama chama chake hicho ulifuatiwa mara baada ya kushindwa kuchaguliwa na chama hicho kuwa mgombea wa urais mwezi uliopita.

Asante kwa kufuatilia tovuti yetu hii, lakini kumbuka kuwa endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu unaweza kuwasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu zifuatazo ; 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment