Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Sunday, 30 August 2015

ENDAPO LOWASSA ATAFANIKIWA KUWA RAIS SERIKALI YAKE ITAYAFANYA HAYA KATIKA SEKTA YA AFYA...


Jana Agosti 29, 2015 UKAWA walizindua kampeni zao jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Jangwani na mgombea urais wa umoja huo Mh: Edward Lowassa alizungumza na wakazi wa jiji hilo japo ilikuwa ni kwa ufupi, lakini kuna mambo mengine wameyachapisha kwenye blog ya chama cha CHADEMA nimeona nikuletee huu mpango wao kuhusu sekta ya afya.

Endapo Mh. Edward Lowassa atakuwa rais serikali yake itafanya haya yafuatayo kuhusu sekta ya afya: 


Afya na tiba ya kila Mtanzania itagharamiwa kupitia bima za gharama nafuu na mifuko ya hifadhi ya jamii

Tutaimarisha afya ya msingi pamoja na kinga kupunguza gharama za tiba.


Serikali itahakikisha kuna uwiano na upatikanaji wa watumishi wa afya katika kada mbalimbali ili kuleta tija na huduma stahiki.


Itaimarisha miundombinu ya afya pamoja na kujenga hospitali za kisasa ili kusogeza huduma za afya karibu na jamii na pia kuepukana na tiba za nje ya nchi.


Tutarejea kwa lengo la kuboresha maslahi na vitendea kazi katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na nyumba na usafiri.


Tutathibiti ongezeko la gharama za huduma za afya bila kuathiri uendeshaji wa watoaji huduma za afya kama vile serikali na hospitali za sekta binafsi.

No comments:

Post a Comment