Thursday, 13 August 2015

EPUKA MAGONJWA YA MOYO KWA KUFANYA HAYA

Hivi sasa magonjwa ya ysiyoambukiza hususani ya moyo yamekuwa yakishika kasi na kusumbua watu wengi kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Magonjwa ya Moyo nchini India, watu milioni 2.4 hufariki dunia kila mwaka kutokana na magonjwa ya moyo, huku sehemu kubwa yakichakiwa na mitindo ya kimaisha ambayo ni pamoja na kuishi na sonono yaani stress, kutokula kwa kuzingatia taratibu za afya pamoja na kukoosa usingizi kwa muda mrefu.

Hata hivyo kuna njia ambazo huweza kumsaidia mtu kuepukana na magonjwa ya moyo, hii ikiwa ni pamoja na namna ya mpangilio wa vyakula sambamba na ufanyaji wa mazoezi.

Unaweza kuepuka magonjwa ya moyo kwa kupendelea kula matunda, mboga za majani pamoja na vyakula vya nafaka ambavyo husaidia kuondoa hatari ya kupata magonjwa ya moyo.

Kuepuka matumizi ya sigara na tumbaku, ambayo yote huweza kuchangia mhusika kuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo. Hivyo endapo umekuwa ni mtumiaji wa sigara au tumbaku ni vyema ukafanya maamuzi ya kuacha mara moja ili kujiondoa katika hatari ya kupata magonjwa haya ya moyo.

Epuka kuwa na uzito kupita kiasi, hali hii huweza kuchangia mwili kulundikana na mfuta hatari yaani cholesterol, ambayo huwa ni hatari kwa afya ya moyo, hivyo ni vizuri ukajenga mazoea ya kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara ili kuepuka kuwa na uzito uliokithuri.

Punguza matumizi ya chumvi kupita kiasi, ulaji wa chumvi kupita kiasi huchangia msukumo wa damu kuwa juu zaidi ambayo ni moja ya sababu inayoweza kuchangia mhusika kuanza kukubwa na tatizo la shinikizo la damu. Pia epuka vyakula ambavyo vimesindikwa kwa chumvi nyingi.

Jitahidi kulala kwa muda wa kutosha angalau masaa 7 hadi 8 kwa siku, kukosa usingizi huweza kusababisha mtu kukosa furaha na kuwa mchangamfu na hata shambulio la moyo, kulala usingizi mzuri hutengeneza mtu kuwa na mchangamfu na uwezo mzuri wa kupambanua mambo.

Jambo la muhimu pia ni kuepuka msongo wa mawazo au kukabiliana na msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo (stress) huweza kusababisha shambulio la moyo (heart attack) na mara nyingine hata kifo. Kufanya mazoezi ni moja ya njia inayoweza kukusaidia kupunguza msongo wa mawazo.

Pamoja na hayo yote lakini kumbuka kwamba ni muhimu sana kujenga tabia ya kufanya uchunguzi wa afya yako mara kawa mara kwa kuangalia msukumo wako wa damu kama upo sawa, na kuhakikisha hauna kiwango cha sumu mwilini pamoja na kuepukana na mgonjwa kama kisukari.

Je, unasumbuliwa na magonjwa sugu? Kama jibu ni ndio basi hakikisha unafika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam ambapo utapata nafasi ya kukutana na mtaalam wa tiba asili, Dk Abdallah Mandai na kupatiwa dawa zisizo na kemikali zitokanazo na mimea mbalimbali na matunda. Pia unaweza kumpigia simu Dk Mandai kwa namba zifuatazo 0653 163 838, 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment