Tuesday, 11 August 2015

FAHAMU UZURI NA FAIDA ZA KULA MAGIMBI KWA AFYA YAKO

Magimbi ni moja ya chakula chenye asili ya mizizi ambacho hupatikana sehemu mbalimbali za nchi hii, ikiwa ni pamoja na Iringa na Mbeya.

Magimbi huhitaji maji mengi wakati wote ili yaweze kustawi, hivyo kutokana na sababu hiyo mara nyingi kilimo cha magimbi kimekuwa kikifanyika sana mabondeni ambapo huwa na maji mengi.

Magimbi yanamsaada mkubwa kwa mlaji kwani husaidia sana kujenga mfumo wa umeng'enyaji chakula kuwa vizuri zaidi hii ni kutokana na kuwa na nyuzinyuzi nyingi yaani 'fiber'. Kufuatia hali hiyo pia ulaji wa magimbi huwa na nafasi kubwa na nzuri ya kusafisha tumbo.

Aidha, magimbi pia yana nafasi ya kuimarisha kinga za mwili kwa mlaji, hii ni kutokana na kuwa na vitamin C ndani yake.

Hayo ni machache tu kuhusu magimbi, lakini naomba nikupe nafasi ya kuyafahamu mengi zaidi kwa kumsikiliza Tabibu Abdallaha Mandai akielezea zaidi kuhusu faida zake.

Bonyeza 'play; ili kusikiliza tafadhali


No comments:

Post a Comment