Friday, 14 August 2015

HAYA NDIYO ALIYOYASEMA MREMA KUHUSU LOWASSA KUWA MGOMBEA WA UKAWA

Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha TLP , Augustino Lyatonga Mrema
Mwenyekiti wa taifa wa TLP Augustine Mrema amewatahadharisha watanzania kuwa macho juu ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao umepoteza mwelekeo na kuyumba kisiasa na kudai kuwa hawafai kuingia ikulu na kuongoza nchi.

Mrema ametoa tahadhari hiyo katika eneo la njiapanda baada ya kurejea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Moshi kuchukua fomu za kugombea ubunge katika jimbo la Vunjo huku akisindikizwa na wafuasi wake.

Amesema, kitendo cha ukawa kumkashifu hadharani waziri aliyestaafu Mh Edward Lowasa kuwa ni fisadi na baadaye kumpokea na kumteua kuwa mgombea wa urais UKAWA imeonyesha udhaifu mkubwa na kwamba watanzania wa sasa si wakuburuzwa.

Mh. Mrema amesema kuwa haiwezekani mtu alieachwa na chama na kuonekana hafai kutokana na tuhuma za ufisadi kicha CHADEMA ndio wakaona anafaa kuwa mgombea huko ni kuonyesha kutokuwa na msimamo ndani ya hivyo ni vigumu kuwapa uongozi wa nchi.

Source: EATV

No comments:

Post a Comment