Thursday, 6 August 2015

HAYA NDIYO MAMBO YA TEKNOLOJIA KUTANA NA HILI LORI LENYE TV NYUMA INAYOONESHA KILA KITU MBELE NA KUMRAHISHIA WA NYUMA KU-OVERTAKE(VIDEO)

Kweli teknolojia imeendelea kukua karibu kila siku, huku wanasayansi wakijitahidi kuumiza vichwa ili kubuni na kugundua vitu mbalimbali.

Leo nimepata bahati ya kuifahamu hii teknolojia mpya ya haya malori yenye TV nyuma ambayo huweza kumuonesha dereva wa gari linalokuja nyuma kila kitu kinachoendelea mbele na hivyo kumrahisishia dereva wa nyuma ku-overtake kwa urahisi na kuepuka ajali.

Kimsingi ajali za barabarani zimekuwa ni tatizo katika nchi mbalimbali duniani hasa nchi zetu hizi zinazoendelea.

Lakini kampuni ya Samsung imeamua kuja na haya malori ambayo yamefungwa 'screen' nyuma ambayo humuonesha dereva atakayekuwa nyuma ya lori hilo kila kitu kinachoendelea mbele na hivyo kumrahisishia hata ku- overtake kwa sababu atakuwa anaona vizuri kilichopo mbele.

Jamaa kashaona mbele vizuri kupitia TV ya kwenye lori sasa anaamua ku-overtake
Teknolojia hiyo inahusisha utumiaji wa kamera maalum ambazo zimefungwa mbele ya lori na kuonesha TV kubwa inayokuwa sehemu ya nyuma ya lori.
Muonekano wa nyuma kwenye lori hizo upo hivi kuna hiyo TV kubwa kabisa
 Wataalam hao wanasema kuwa TV hiyo imetengenezwa kwa vioo maalum na hivyo kuifanya iwe imara na kutovunjika kwa urahisi.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa  TV zilizofungwa nyuma ya malori hayo zinauwezo wa kuonekana vizuri hata nyakati za usiku pia.

Aidha, Samsung wanasema teknolojia hiyo itasaidia kuzuia ajali za aina mbalimbali za barabarani ikiwa zile zinazosababishwa na maamuzi ya wakati wa ku-overtake au ajali zinazotokana na malori kufunga break za ghafla kutokana na wanyama au watu kuvuka barabara ghafla.
 Hadi sasa magari hayo tayari yamefanyiwa majaribio nchini Argentina ambayo ni moja ya nchi zinazoongoza kwa ajali za malori na hadi sasa wengi wameisifu sana teknolojia hiyo.

Inaelezwa kuwa kilichobaki hadi sasa ni kufanya maboresho na kisha kuomba kibali rasmi katika nchi mbalimbali ili kuweza kupata baraka ya utumiaji wa teknolojia hiyo.

Hapa chini nimekuwekea video ya namna malori yenye teknolojia hiyo yanavyofanya kazi yakiwa barabarani. Karibu utazame.

No comments:

Post a Comment