Monday, 17 August 2015

HAYA NDIYO MANENO YA NCHIMBI BAADA YA UKIMYA WAKE

Dk. John Nchimbi
Baada ya kuwepo kwa tetesi kwamba Dk John Nchimbi hakuridhishwa na ule mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia CCM uliofanyika mjini Dodoma hatimaye Dk John Nchimbi, ameibuka na kudai kuwa, hana kinyongo na yaliyotokea Dodoma huku akionesha kuwashangaa wanaoendelea kunung’unika, akisema watu wa aina hiyo hawakuwa pamoja na chama.

Hayo aliyasema mwishoni mwa wiki wakati wa Baraza Kuu la UVCCM jijini Dar es Salaam, ambapo amesema sasa si wakati wa kuendelea kuwa na makundi, bali kujenga umoja kwa lengo la kukipa chama ushindi.

Aidha, Nchimba amesisitiza kuwa hana kinyongo, bali anaunganisha nguvu zake na wana CCM wengine ili kuhakikisha ushindi wa Dk John Magufuli, aliyekabidhiwa jukumu la kupeperusha bendera ya CCM katika urais.

Karibu unaweza kutangaza nasi kwa gharama nafuu sana wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment