Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 31 August 2015

HII NDIYO SIRI YA KIMATIBABU INAYOPATIKANA NDANI YA MAJANI YA NANASI

Majani ya nanasi yakiwa tayari yamesagwa
Habari za Jumatatu mpendwa mfuatiliaji wetu wa www.dkmandai.com leo ni siku nzuri tena ambapo tunaendelea kufahamishana kuhusu mimea tiba mbalimbali. 

Ndani ya weekend hii nashukuru sana kwani nimepokea maswali mengi sana kupitia namba  ya simu ya 0769 400 800 ambapo wengi waliuliza kwanini tumekuwa tukizungumzia sana faida za nanasi kama tunda na juisi yake, lakini hatujawahi kuongelea kabisa kuhusu yale majani yake?
 

Hivyo nimeona nitumie nafasi hii kuwajibu wale wengi waliohitaji kujua faida za majani ya mnanasi katika tiba.

Kama umekuwa ukifuatilia tovuti hii naamini utakuwa unafahamu kwamba mara kadhaa tumeshazungumzia umuhimu wa matumizi ya tunda la nanasi kiafya.

Lakini leo Mandai Herbalist Clinic tunakufahamisha matumizi ya majani au matawi ya mmea wenyewe wa nanasi.

Majani haya yanauwezo wa kuwasaidia sana wale wenye matatizo ya figo, kujaa kwa miguu au miguu kuwaka moto na kupasuka.

Majani haya pia yanauwezo wa kuwasaidia wale wenye shida ya kuumwa na kichwa mara kwa mara.

Unachopaswa kufanya ili majani haya yawe msaada kwako kama tiba ni kuhakikisaha unapata majani matano ya mmea huu wa nanasi kisha yasage na kuchanganya kwenye maji ya moto na baadaye chuja.

Baada ya hapo subiri maji hayo yenye mchanganyiko wa majani ya nanasi yapoe kisha mhusika yaani mgonjwa atumie kiasi cha nusu glasi asubuhi na jioni.


Kwa maelezo na ushauri zaidi unaweza kuwasilina na Tabibu Abdallaha Mandai  kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment