Friday, 7 August 2015

HIVI UNAJUA KUWA KUKOSA KWAKO USINGIZI KUNA ATHARI KIAFYA?

Usingizi ni moja ya kitu muhimu sana kwa afya zetu wanadamu na wanasayansi wanaamini kuwa kulala kunasaidia katika kujenga seli mpya za ubongo.

Wanasayansi wanaeleza kwamba, usingizi husaidia kuzalisha upya celi za ubongo ambazo nazo hujenga kemikali inayojulikana kama ‘myelin’ ambayo ni muhimu katika kulinda ubongo wetu kwa ambavyo unafanya kazi.

Ni wazi kuwa binadamu huhitaji kulala ili kupumzika pamoja na kuufanya ubongo kufanya kazi yake inavyopaswa, lakini pia kumekuwepo na mambo ya kibayolojia yanayofanyika tunapokuwa tumelala ikiwa ni pamoja na hili la kujenga seli mpya za ubongo.

Aidha, watafiti wanabainisha kuwa mtu anapokosa usingizi huweza kupelekea akapata maradhi ya ubongo yanayoathiri seli.

Mbali na hayo, watafiti pia wanataka kuchunguza endapo ikiwa vijana wanapokosa usingizi wakati wa ukuaji wao ni kwa kiasi gani huweza kuathiri ubongo katika siku za usoni.

Miongoni mwa faida za usingizi ni pamoja na kuwa na umuhimu katika mfumo wa neva mwilini, hivyo kumfanya mhusika kuweza kufanya kazi vyema, hali kadhalika usingizi pia husaidia katika uzalishaji wa homoni zinazowafanya watoto na vijana kukuwa.

Pamoja na hayo, mtafiti na Dk Cirelli alisema kuwa "kwa muda mrefu, watafiti wa usingizi wamekuwa wakilenga tofauti iliyopo kati ya seli za neva wakati wanyama wanapokuwa hawajalala na wakati wamelala, lakini kwa sasa ni bayana kuwa seli nyingine kwenye mfumo wa neva hubadilika kutokana na usingizi.” alisema.

Wanasayansi wanasema kuwa kufanya kazi katika muda usio wa kawaida kikazi au katika mazingira yaliyo ya upweke kunaweza kuzeesha ubongo na kufanya uwezo wa utendaji kuwa duni, huku wakiongeza kuwa miili na akili zimejengwa kwa kufanya kazi mchana na kulala nyakati za usiku.

Mbali na hayo pia kwa mujibu wa utafiti ulioelezwa katika jarida la ‘Occupational and Environmental Medicine’ kuwa iwapo kazi za kupokezana, mfano nyakati za usiku zitafanywa kwa takriban miaka kumi mfululizo zitazeesha ubongo kabla ya wakati wake.

Karibu sana Mandai Herbalist Clinic upate suluhisho la magonjwa sugu tiba zetu ni za mimea, matunda, nafaka na mitishamba tunafanya kazi kila siku Jumatatu hadi Jumapili. Kumbuka kuwa tunapatikana Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam na kwa mawasilano zaidi tutafute kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800, 0652 163 838 barua pepe ni dkmandaitz@gmail.com 

No comments:

Post a Comment