Friday, 14 August 2015

HIZI NDIO DALILI ZA TATIZO LA UVIMBE KWENYE KIZAZI

Nimekuwa nikipokea maswali mengi sana karibu kila siku kutoka kwa watu mbalimbali wakihitaji kufahamu kuhusu mimea tiba na baadhi ya magonjwa pia, lakini moja ya swali ambalo nakiri kulipokea kutoka kwa watu wengi ndani ya wiki hii ni hili la kuhusu tatizo la uvimbe kwenye kizazi, wengi walihitaji kuzijua dalili za tatizo hili.

Lakini kwanza kabla ya kuzifahamu dalili ni vyema tufahamu kuwa uvimbe kwenye mfuko wa kizazi ni nini? Tatizo hili hujulikana kama 'fibroid'. Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi.

Tatizo hili huweza kumpata mwanamke yeyote katika maisha yake, lakini hasa huwapata zaidi wanawake walio katika umri wa miaka ya uzazi. Pia ni tatizo ambalo linashuhudiwa sana katika jamii kwa sasa.

Tatizo hili mara nyingi huwa halioneshi dalili za moja kwa moja hasa uvimbe unapokuwa mdogo, hivyo dalili zake hutegemea sehemu ulipo kwenye mfuko wa uzazi na pia ukubwa wake.

Pale inapofikia hatua ya kuonesha dalili mhusika (mwanamke) hutokwa na damu nyingi kwa muda mrefu wakati wa hedhi ikiambatana na mabonge mabonge isivyo kawaida, au kutokwa damu isiyo ya kawaida katikati ya mwezi au hedhi zisizokuwa na mpango. Kufuatia hali hiyo baadhi ya wanawake hujikuta wameingia katika tatizo la upungufu wa damu mwilini 'anemia.'


Dalili nyingine ni kupata maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi, maumivu makali ya tumbo, maumivu wakati wa tendo la ndoa, maumivu ya mgomgo na kukojoa mara kwa mara kwani uvimbe hukandamiza kibofu cha mkojo.

Dalili nyingi za 'fibroid' ni mwanamke kushika mimba lakini huharibika na kuishia kutoka na wengine hushindwa kabisa kushika mimba na wakati mwingine kuwa wagumba.

Tatizo hili pia huweza kuambatana na matatizo ya kukosa choo, matatizo ya figo

Kama unasumbuliwa na tatizo hili au umeona dalili moja wapo kati ya hizo hapo juu ni vyema ukawahi kwenye kituo cha afya kilicho karibu na wewe au unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic kwa ajili ya vipimo na matibabu zaidi. Wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment