Saturday, 8 August 2015

HUU NDIO UMUHIMU WA VIAZI VITAMU KWA AFYA YAKOHabari za leo mpendwa msomaji wa www.dkmandai.com karibu tena katika siku hii nzuri ya Jumamosi ya Agosti 8, 2015 ikiwa ni sikuku ya wakulima.

Leo ningependa kuzungumzia kuhusu viazi vitamu, viazi ambavyo vinpatikana kwa wingi sana hapa nchini kwani karibu mikoa mingi hujihusisha na kilimo hiki.

Viazi vitamu ni miongoni mwa vyakula vinavyo stawisha mwili hasa ngozi pasipo kujali ni ya mwanamke au mwanaume.

Viazi vitamu vina vitamin A na C ambazo zote mbili zinasaidia kwenye kustawisha ngozi ya mwanadamu na kuifanya kuwa nzuri.
Kuhusu Vitamin C yenyewe huisaidia ngozi kuwa nyororo na kwa upande wa Vitamini A hii husaidia kupigana na uharibifu wa ngozi kutokana na magojwa mbalimbali. Mfano upele.

Hivyo katika maadhimisho haya ya nane leo ni vyema pia watu wakahamasika kuanza kupanda viazi katika maeneo yao ili kuzipata faida hizo kiafya, lakini hata kiuchumi pia ikibidi.

Karibu sana Mandai Herbalist Clinic upate suluhisho la magonjwa sugu tiba zetu ni za mimea, matunda, nafaka na mitishamba tunafanya kazi kila siku Jumatatu hadi Jumapili. Kumbuka kuwa tunapatikana Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam na kwa mawasilano zaidi tutafute kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800, 0652 163 838 barua pepe ni dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment