Saturday, 1 August 2015

IPATE HII TAARIFA YA MATUMAINI KWA DUNIA KUHUSU UGONJWA WA EBOLA

Ugonjwa wa ebola ni ugonjwa ambao ulisababisha vifo vya watu wengi hasa katika nchi za Afrika Magharibi


Kufuatia kuibuka kwa ugonjwa huo hatari wanasayansi na watafiti mbalimbali walikuwa wakiendelea kutafuta namna ya kuweza kukabiliana na ugonjwa huo na hatimaye kuna haya matokeo  mazuri yametoka.

Taarifa zinasema kwamba Shirika la Afya Duniani (WHO), limesifia matokeo ya chanjo mpya  ya ugonjwa wa Ebola, ambayo inatoa asilimia 100% ya kinga baada ya majaribio yake nchini Guinea.

Kufuatia kupatikana kwa matokeo hayo, WHO imesema kuwa ulimwengu unakaribia zaidi kupata chanjo mpya dhidi ya ugonjwa huo hatari wa Ebola.

Chanjo dhidi ya ebola
Inaelezwa dawa ya chanjo hiyo ilijaribiwa kwa maelfu ya watu, mara tu mtu mmoja aliyekuwa karibu nao alipoambukizwa ugonjwa huo, lakini baada ya kutibiwa kwa siku kumi hakuna hata mmoja wao alikuwa ameambukizwa ugonjwa huo.

Hata hivyo pamoja ya kuwa chanjo hiyo bado haijaidhinishwa rasmi ama kupewa leseni, lakini tayari maandalizi yanafaywa ili isambazwe kote Duniani.

Zaidi ya watu elfu kumi na moja wamefariki kutokana na ugonjwa huo wa ebola, tangu ulipolipuka nchini Guinea mwezi Disemba mwaka 2013.

Unaweza kutangaza na tovuti hii sasa wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment