Friday, 14 August 2015

JAMAA ALIMBAKA MTOTO NA AKAMUAMBUKIZA UKIMWI, MAHAKAMA HAIKUMUONEA HURUMA KABISA IKAFANYA MAAMUZI YAKE. YAPO HAPA

Mahakama moja nchini Kenya imemhukumu mwanaume mmoja kifungo cha miaka 130 jela kwa kumbaka na kumuambukiza mtoto mwenye umri wa miaka 9 UKIMWI.

Katika kikao hicho Mahakama kuu ya Kenya mjini Kisumu imemkuta  na hatia bwana John Okewo mwenye umri wa miaka 25 na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 9 ambaye jina lake limehifadhiwa

Hakimu mwandamizi Aswani Opande alimkuta na hatia bwana Okewo kwa kumbaka mtoto huyo na akamhukumu kifungo cha miaka 100 jela.

Katika shtaka la pili hakimu huyo mkuu wa eneo la Tamu lililoko Muhoroni alimhukumu mstakiwa kifungo cha miaka mingine 30 kwa kumuambukiza msichana huyo mwenye umri wa miaka 9 ugonjwa wa Ukimwi.

Hakimu alimpata na hatia bwana Okewo kutokana na kukiri makosa yake mwenyewe.

Upande wa mashtaka unasema kuwa bwana Okewo alimpa mtoto huyo pipi na biskuti mnamo tarehe 27 mwezi Machi kabla ya kumdanganya hadi akaingia chumbani mwake.

Kwa upande wa mtoto aliyetendewa tukio hilo baya anasema alimtambua mshtakiwa kuwa mtu aliyemnunulia pipi na ''kumlalia'' Kwa sasa mtoto huyo anaendelea na matibabu maalum ya wanawake baada ya kujeruhiwa katika tukio hilo.

Mbali na hayo mshitakiwa alipopewa fursa ya kujitetee, mshtakiwa aliomba asamehewe kwani ni ''shetani aliyemdanganya'' kutenda maovu hayo. Hata hivyo Hakimu akakataa kabisa kumuonea huruma na akamhukumu kifungo cha miaka 130 jela ili iwe funzo kwake na kwa wengine wenye mawazo potofu kama yake na alipewa siku 14 kukataa rufaa.

Unaweza kutangaza na tovuti hii kwa gharama nafuu sana tupigie simu sasa kwa namba za simu zifuatazo 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmaandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment