Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 31 August 2015

JESHI LA POLISI LIMEFANIKIWA KUWAKAMATA WASHUKIWA 38 WA UGAIDI

Jeshi la Polisi nchini wamefanikiwa kuwakamata washukiwa 38 wa ugaidi ambao wanauhusiano na kundi la kigaidi lililofanya mashambulio katika vituo kadhaa vya polisi nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova alisema washukiwa hao walikamatwa wakiwa na bunduki kumi na risasi 387, mabomu ya kurushwa kwa mkono maarufu kama grunedi na vifaa vya kutengenezea mabomu.

Katika mkutano wake huo na wanahabari  Kamanda Kova, aliwaonyesha waandishi wa habari silaha walizonasa kutoka kwa washukiwa hao.

Kamanda Kova amesema uchunguzi wa awali, umebainisha kuwa kuna uwezekano  kuwa waliokamatwa wana mitandao mingine ya kigaidi.
 

Aidha, Kamanda Kova amesema washukiwa hao walikamatwa baada ya operesheni kali iliyofanywa katika miji ya Lindi na Tanga.

Bila kutaja majina yao, Kova amesema kuwa miongoni mwa wa waliokamatwa ni wavulana walio na umri wa chini ya miaka 17.
 

Itakumbukwa kwamba Julai 15, mwaka huu watu waliokuwa wamejihami walishambuio kituo cha polisi Dar es Salaam na kuwauawa maafisa saba wa polisi na raia kadhaa, kabla ya kutoweka na idadi ya silaha isiyojulikana.

Katika tukio lingine lililofanana na filamu, watu waliokuwa wamejihami walishambulia kituo cha polisi katika wilaya ya Bukombe, eneo la Geita na kuwauawa maafisa wawili wa polisi.


Hata hivyo, idara ya jeshi la polisi, halijasema ni lini washukiwa hao walikamatwa au siku watakayofikishwa mahakamani.

Source: BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment